Tuesday, 12 June 2018

Rotaractors - young professionals wafadhili mafunzo ya Hedhi Salama kwa walimu na wanafunzi wasioona katika shule ya Toa Ngoma




Walimu wa shule ya Toa Ngoma kitengo cha elimu maalum, walifanikiwa kuchapisha vitabu na michoro ya Hedhi Salama katika maandishi ya braille, hii ikiwa ni moja ya shughuli zilizofadhiliwa na rotaractors - young professionals
Dokta Aidat akimfafanulia kwa kina Mwl. Catherine kuhusu mfumo wa uzazi wa mwanamke. Mwalimu Catherine ni mwalimu wa elimu maalumu shuleni Toa Ngoma

Dokta Atu, akiwafafanulia kwa kina Mwl Flora na Mwl Subira mchoro wa mfumo wa uzazi wa mwanamke ambao upo katika maandishi ya braille

Dokta Aidat akiendelea kufundisha kuhusu Balehe na Hedhi Salama
Omary mmoja wa wakufunzi na mwalimu wa kujitolea wa Hedhi Salama akiuliza swali wakati wa mafunzo ya Balehe na Hedhi Salama
Dr. Atu akiendelea kufundisha kuhusu balehe na Hedhi Salama
Mwenyekiti wa Chama cha wasiona Tanzania akitoa shukrani zake za dhati kwa timu nzima ya Hedhi Salama na Rotaractors ambao ni wafadhili wa mafunzo haya
Rehema Darueshi, mkufunzi wa Hedhi Salama na Mwalimu wa shule ya Toa Ngoma akipokea cheti chake baada ya kuhitimisha mafunzo
Flora Dea, Mkufunzi wa Hedhi Salama na mwalimu wa shule ya Kimanzi chana akipokea cheti chake baada ya kuhitimisha mafunzo
Wakufunzi wote wa Hedhi Salama walipata fursa ya kujifunza jinsi ya kutengeneza taulo za kike, Mwalimu Subira alitengeneza taulo ya kike na kuamua kuiita Subira pad
Mwalimu Ally pia alitengeneza taulo ya kike na kuamua kuiita Ally pad
Mwalimu Flora akijibu swali
Wakufunzi wa Hedhi Salama wakionyesha taulo za kike walizozitengeneza
Muongozo wa ufundishaji juu ya Balehe na Hedhi Salama ulichapishwa kutoka kwenye maandishi ya wanaoona kwenda kwenye maandishi ya wasioona

0 comments: