Tuesday, 12 December 2017

Ufunguzi wa kisima cha maji katika shule ya msingi King'ong'o waambatana na mafunzo ya Hedhi SalamaFeza Alumni Foundation wajenga kisima cha maji kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi King'ongo'. Maji haya pia yanatarajiwa kutumiwa na wananchi waishio maeneo yanayoizunguka shule hiyo
Kisima hiki ni ushahidi tosha kwamba wana Feza wanatambua umuhimu kwa kuzisaidia jamii hasa zile zenye kipato duni. Shule ya King'ong'o ni shule iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na imekua ikikabiliwa na changamoto ya kukosa maji jambo lililokua likihatarisha afya ya wanafunzi hao
Elimu juu ya Hedhi Salama ni moja kati ya mada zilizofundishwa kwa wanafunzi wakati wa ufunguzi wa kisima shuleni hapo
Wanafunzi, wana Feza, walimu na watoa mada kutoka Kasole Secrets wakifurahia ufunguzi wa kisima ambapo kimewasha taa kubwa ya matumaini ya kupunguza usumbufu na kuimarisha afya ya wanafunzi na wana Kingo'ong'o kwa ujumla
Wana Feza wakizungumza na wanafunzi kuhusu umuhimu wa usafi na nini kinapaswa kufanyika ili kudumisha usafi
Wanafunzi wakifanya mchezo wa kuvunja ukimya moja ya mbinu ya kujifunza kuhusu Hedhi Salama
Mchezo huu wa kuvunja ukimya huwajengea wanafunzi ujasiri bali pia huwafanya wafikiri kwa makini kila wanapotaka kujibu maswali

Wanafunzi wakiwaangalia na kuwasikiliza kwa makini wenzao wanaocheza mchezo wa kuvunja ukimya
Mwanafunzi akianisha mabadiliko ya mwili yanayotokea katika mwili wa mtoto wa kiume
Mkufunzi Bi. Hyasintha Ntuyeko akiwauliza wanafunzi swali
Wanafunzi wakinyoosha mikono kwa nguvu zote tayari kwa kujibu swali waliloulizwa
Mwanafunzi akiainisha mabadiliko ya mwili yanayotokea katika mwili wa mtoto wa kike
Mwanafunzi akiendelea kuainisha mabadiliko yanayotokea katika mwili wa mtoto wa kiume
Dr. Aidat, akifafanua kwa kina kuhusu mabadiliko ya mwili yanayotokea kwa mtoto wa kiume na wa kike na nini husababisha mabadiliko hayo
Wanafunzi wamkisikiliza Dr. Aidat kwa makini

0 comments: