Monday, 7 November 2016

Wanafunzi wamuonyesha Mganga Mkuu wa wilaya, Dr. Wonanji jinsi ya kutengeneza dawa ya chooni

Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Matemboni, akimuonyesha mganga mkuu wa wilaya ya Moshi, Dr. Wonanji, pamoja na jopo lake jinsi ya kutengeneza dawa ya kutengenezea choo kwa kutumia vumbi la mkaa, majivu na chumvi
Mwanafunzi Robert Shayo kutoka shule ya msingi Matemboni, akionyesha vipimo vya mikono, vinavyohitajika ili kuweza kuwianisha mchanganyiko wa dawa hiyo ya kusafishia choo.

Mwanafunzi Leah Tarimo, kutoka shule ya msingi matemboni akichanganya mchanganyiko huo uliokwisha pimwa vizuri na mwanafunzi mwenzake Robert, tayari kabisa kwa kuanza kutumika katika shughuli za usafi
Mwanafunzi Leah, akiwa ameshikilia fagio lake alilolitengeneza mwenyewe, tayari kabisa kuonyesha jinsi anavyoweza kutumia dawa hiyo kusafisha choo.
Mwanafunzi Robert, akionesha jinsi anavyoweza kutumia kibuyu chirizi kusafisha vizuri mikono yake mara baada ya kutoka chooni. Kibuyu hiki chirizi kimetengenezwa na wanafunzi wenyewe, ikiwa ni moja ya stadi walizofundishwa katika program ya hedhi salama shuleni hapo0 comments: