Monday, 25 July 2016

MUONGOZO WA KUFUNDISHIA HEDHI SALAMA WATUMIKA MOSHI PIA

Muongozo wa mafunzo juu ya hedhi salama na ukuaji sasa umeongeza wigo kwa kutumika pia Moshi, mbali na hapo awali ulipokua ukitumika Dar-es-salaam na Ifakara. Muongozo huu ambao umeandiwa na muuguzi Jo Rees na kuweza kufanya vizuri sana katika shule za msingi na za sekondary nchini Ethiopia, kampuni ya Kasole secrets iliona ni vyema kuutumia pia muongozo huo katika program zao za hedhi salama nchini Tanzania. Bi Hyasintha Ntuyeko anasema ni mwaka sasa tangu waanze kuutumia muongozo huo, ambao ulitokea kupendwa sana na wanafunzi na walimu pia. Sasa muongozo huo utatumiwa tena kufundishia shule za moshi vijijini ambapo shirika la Msichana Inititive, Childreach na Tuleane watafundishwa jinsi ya kuutumia muongozo huu.

0 comments: