Sunday, 31 January 2016

PAMOJA CLUBS PIA ZAANZISHWA WILAYANI IFAKARA

Bi Regina Kway, mwanafunzi wa udaktari katika chuo cha mtakatifu Francis kilichopo Ifakara-Morogoro, akiongea na wanafunzi wa sekondari kuhusu hedhi salama na balehe

Dr. Eveline Emmanuel Sikahanga, akisikiliza kwa makini wanafunzi wa secondary wilaya Ifakara wakijielezea jinsi wanavyoelewa juu ya hedhi salama na balehe
Bi. Irene Ndeki, mwanafunzi wa udaktari katika chuo cha mtakatifu Francis kilichopo Ifakara akizungumza na wanafunzi juu ya hedhi salama na balehe
Wanafunzi wakiuliza maswali mbalimbali juu ya hedhi salama na balehe
Bi. Regina akitoa hadithi yake juu ya hedhi yake ya kwanza, nini kilitokea na nini alifanya, story ya Regina iliwafanya wanafunzi wengi wahadithie hadithi zao pia

Bi. Irene Ndeki akifafanua kwa michoro katika kujaribu kujibu maswali ya wanafunzi wake

Wanafunzi wakiwa katika hamasa kubwa na utayari wa kuunda kikundi cha hedhi salama shuleni wao huku wakiahidi kuhudhuria bila kukosa


Dr. Eva akijadiliana na mabinti juu ya uelewa wao kuhusu hedhi salama na ukuaji
Bi. Irene Ndeki, akiwa katika moja ya mijadala iliyowafanya wanafunzi wacheke na kuamua kuzungumza mengi zaidi kuhusu hedhi salama na balehe, huku wakitoa hadithi mbalimbali na mikasa mbalimbali
Watoto wakiume wakizungumza na Dr.Eva, kuhusiana na balehe, wanafunzi hawa walikua na maswali mengi mno kuhusiana na balehe
Bwana Nobert Sezari mwanafunzi wa udaktari katika chuo cha mtakatifu Francis akizungumza na wanafunzi wa kiume kuhusu balehe
Bwana Kelvin Kafumu, mwanafunzi wa udaktari kutoka chuo cha mtakatifu Francis akizungumza na wanafunzi wa kiume juu ya balehe, wanafunzi wakiume walionesha kuvutiwa zaidi na kutaka kufahamu zaidi juu ya balehe

Mijadala ya vikundi kwa vikundi ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kujua uelewa wa wanafunzi wa kike kwa wakiume kuhusu balehe na hedhi salama, pia ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kujua chagamoto za mwanafunzi mmoja mmoja na utayari wao kuunda club shuleni hapo na kuleta mabadiliko ya kweli katika kuhakikisha wanazifikia ndoto zao

Team Kasole-Ifakara ikitoa tathimini ya yale waliyoyasikia katika mijadala na wanafunzi na nini kifanyike katika kuboresha clubs za hedhi salama na balehe mashuleni
Wanafunzi na Dr. Eva katika pozi

0 comments: