Friday, 22 January 2016

PAMOJA CLUBS KATIKA MASHULE ZAPOKELEWA KWA SHAUKU KUBWA Wanafunzi wa kike na wakiume wakikimbilia mbele ili waweze kupata fursa ya kua moja kati ya wanafunzi watakao unda club ya Pamoja Tanzania yenye lengo la kutoa mafunzo ya ukuaji na hedhi salama huku wanafunzi hao wakihakikisha wanashirikiana kwa pamoja katika kuweka mazingira ya shule hususani vyoo kua visafi wakati woteMjadala wa wanafunzi mmoja mmoja ulioendeshwa na Bi. Hyasintha Ntuyeko, Mkurugenzi mtendaji wa campuni ya Kasole secrets, wenye kulenga kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuweza kujifunza vyema wakiwa kwenye clubs bila kuchekana, kuona aibu au kupeana majina mabaya ya utani ambayo yanaweza kuathiri usikilizaji wao darasani


 Mjadala wa wanafunzi mmoja mmoja ulioendeshwa na Bi. Lilian Benjamin, mwanafunzi kutoka chuo cha udaktari cha Kairuki, wenye kulenga kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuweza kujifunza vyema wakiwa kwenye clubs bila kuchekana, kuona aibu au kupeana majina mabaya ya utani ambayo yanaweza kuathiri usikilizaji wao darasani
Mjadala wa wanafunzi mmoja mmoja ulioendeshwa na Bw. Deusdedith Kapufi, mwanafunzi kutoka chuo cha udaktari cha Kam, wenye kulenga kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuweza kujifunza vyema wakiwa kwenye clubs bila kuchekana, kuona aibu au kupeana majina mabaya ya utani ambayo yanaweza kuathiri usikilizaji wao darasani
 Bwana Deusdedith Kapufi akitoa muongozo kwa wanafunzi, akiwasihi kushirikiana kwa pamoja katika kujifunza wakiwa kwenye clubs, ili waweze kunufaika na mafundisho Bi Lilian Benjamin, ambaye pia ndio mlezi wa club hii katika hii shule akitoa wito wa nidhamu kwa wanafunzi, ili waweze kwenda sawa katika club, Bi Lilian alisisitiza kua angefurahi sana kama wanafunzi wataweka mbele masomo haya ili wayaelewe kwa kina na baadae waje kuwafundisha wenzao ambao hawakupata nafasi ya kua kwenye club hii

Wanafunzi wakijaza mkataba wa makubaliano ya kujiunga na club na kua wasikivu huku wakishirikiana vyema na wanafunzi wenzao pamoja na mlezi wao wa club ili waweze kufikia malengo

0 comments: