Sunday, 31 January 2016

PAMOJA CLUBS PIA ZAANZISHWA WILAYANI IFAKARA

Bi Regina Kway, mwanafunzi wa udaktari katika chuo cha mtakatifu Francis kilichopo Ifakara-Morogoro, akiongea na wanafunzi wa sekondari kuhusu hedhi salama na balehe

Dr. Eveline Emmanuel Sikahanga, akisikiliza kwa makini wanafunzi wa secondary wilaya Ifakara wakijielezea jinsi wanavyoelewa juu ya hedhi salama na balehe
Bi. Irene Ndeki, mwanafunzi wa udaktari katika chuo cha mtakatifu Francis kilichopo Ifakara akizungumza na wanafunzi juu ya hedhi salama na balehe
Wanafunzi wakiuliza maswali mbalimbali juu ya hedhi salama na balehe
Bi. Regina akitoa hadithi yake juu ya hedhi yake ya kwanza, nini kilitokea na nini alifanya, story ya Regina iliwafanya wanafunzi wengi wahadithie hadithi zao pia

Bi. Irene Ndeki akifafanua kwa michoro katika kujaribu kujibu maswali ya wanafunzi wake

Wanafunzi wakiwa katika hamasa kubwa na utayari wa kuunda kikundi cha hedhi salama shuleni wao huku wakiahidi kuhudhuria bila kukosa


Dr. Eva akijadiliana na mabinti juu ya uelewa wao kuhusu hedhi salama na ukuaji
Bi. Irene Ndeki, akiwa katika moja ya mijadala iliyowafanya wanafunzi wacheke na kuamua kuzungumza mengi zaidi kuhusu hedhi salama na balehe, huku wakitoa hadithi mbalimbali na mikasa mbalimbali
Watoto wakiume wakizungumza na Dr.Eva, kuhusiana na balehe, wanafunzi hawa walikua na maswali mengi mno kuhusiana na balehe
Bwana Nobert Sezari mwanafunzi wa udaktari katika chuo cha mtakatifu Francis akizungumza na wanafunzi wa kiume kuhusu balehe
Bwana Kelvin Kafumu, mwanafunzi wa udaktari kutoka chuo cha mtakatifu Francis akizungumza na wanafunzi wa kiume juu ya balehe, wanafunzi wakiume walionesha kuvutiwa zaidi na kutaka kufahamu zaidi juu ya balehe

Mijadala ya vikundi kwa vikundi ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kujua uelewa wa wanafunzi wa kike kwa wakiume kuhusu balehe na hedhi salama, pia ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kujua chagamoto za mwanafunzi mmoja mmoja na utayari wao kuunda club shuleni hapo na kuleta mabadiliko ya kweli katika kuhakikisha wanazifikia ndoto zao

Team Kasole-Ifakara ikitoa tathimini ya yale waliyoyasikia katika mijadala na wanafunzi na nini kifanyike katika kuboresha clubs za hedhi salama na balehe mashuleni
Wanafunzi na Dr. Eva katika pozi

Monday, 25 January 2016

WANAFUNZI WA KIUME WAPOKEA PAMOJA CLUBS KWA SHAUKU KUBWA

 Dokta Aidat Mugula akizungumza na wanafunzi wa kiume walioonyesha shauku kubwa ya kutaka kuelewa zaidi juu ya maswala ya ukuaji
Bi Salma Welele, mwanafunzi kutoka chuo cha udaktari IMTU, akizungumza na mabinti juu ya ukuaji na hedhi salama, mabinti hawa pia hawakutaka kubaki nyuma kwa kuuliza maswali mbalimbali 
Wanafunzi waridhia kujaza form ya kukubali kujiunga na club ya Pamoja Tanzania ili waweze kujifunza kwa kina juu ya ukuaji na hedhi salama
Bi. Dinna Nyirenda, mwanafunzi kutoka chuo cha udaktari cha Kairuki na mlezi wa club akiongea na mabinti juu ya umuhimu wa kujiunga na Pamoja club hapo shuleni 
 Bi. Hyasintha Ntuyeko akiwasikiliza mabinti walipokua wakishirikisha uelewa wao juu ya maswala ya hedhi salama
Wanafunzi waki saini karatasi ya makubaliano kuonyesha utayari wao kujiunga na Pamoja Tanzania club shuleni hapo
 Dokta Aidat Mugula akisikiliza kwa makini maswali kutoka kwa wanafunzi wa kiume
Wanafunzi wakikimbilia mbele kuokota karatasi ili waweze kua moja kati ya wanafunzi watakao chaguliwa kuunda clubs shuleni hapo

 Picha ya pamoja na wanafunzi waliofanikiwa kuunda club ya Pamoja Tanzania
Friday, 22 January 2016

PAMOJA CLUBS KATIKA MASHULE ZAPOKELEWA KWA SHAUKU KUBWA Wanafunzi wa kike na wakiume wakikimbilia mbele ili waweze kupata fursa ya kua moja kati ya wanafunzi watakao unda club ya Pamoja Tanzania yenye lengo la kutoa mafunzo ya ukuaji na hedhi salama huku wanafunzi hao wakihakikisha wanashirikiana kwa pamoja katika kuweka mazingira ya shule hususani vyoo kua visafi wakati woteMjadala wa wanafunzi mmoja mmoja ulioendeshwa na Bi. Hyasintha Ntuyeko, Mkurugenzi mtendaji wa campuni ya Kasole secrets, wenye kulenga kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuweza kujifunza vyema wakiwa kwenye clubs bila kuchekana, kuona aibu au kupeana majina mabaya ya utani ambayo yanaweza kuathiri usikilizaji wao darasani


 Mjadala wa wanafunzi mmoja mmoja ulioendeshwa na Bi. Lilian Benjamin, mwanafunzi kutoka chuo cha udaktari cha Kairuki, wenye kulenga kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuweza kujifunza vyema wakiwa kwenye clubs bila kuchekana, kuona aibu au kupeana majina mabaya ya utani ambayo yanaweza kuathiri usikilizaji wao darasani
Mjadala wa wanafunzi mmoja mmoja ulioendeshwa na Bw. Deusdedith Kapufi, mwanafunzi kutoka chuo cha udaktari cha Kam, wenye kulenga kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuweza kujifunza vyema wakiwa kwenye clubs bila kuchekana, kuona aibu au kupeana majina mabaya ya utani ambayo yanaweza kuathiri usikilizaji wao darasani
 Bwana Deusdedith Kapufi akitoa muongozo kwa wanafunzi, akiwasihi kushirikiana kwa pamoja katika kujifunza wakiwa kwenye clubs, ili waweze kunufaika na mafundisho Bi Lilian Benjamin, ambaye pia ndio mlezi wa club hii katika hii shule akitoa wito wa nidhamu kwa wanafunzi, ili waweze kwenda sawa katika club, Bi Lilian alisisitiza kua angefurahi sana kama wanafunzi wataweka mbele masomo haya ili wayaelewe kwa kina na baadae waje kuwafundisha wenzao ambao hawakupata nafasi ya kua kwenye club hii

Wanafunzi wakijaza mkataba wa makubaliano ya kujiunga na club na kua wasikivu huku wakishirikiana vyema na wanafunzi wenzao pamoja na mlezi wao wa club ili waweze kufikia malengo