Monday, 12 December 2016

Ifakara yapata walimu 31 wa Hedhi Salama

 Jo Rees, nurse mbobezi katika elimu ya afya ya uzazi akiendesha mafunzo ya wakufunzi wa Hedhi Salama katika kijiji cha Ifakara kilichopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Wakufunzi hawa ni wanafunzi wa masomo ya udaktari kutoka chuo cha Mt. Francis, ambao wanategemewa kufundisha kwa kujitolea katika shule za sekondari zilizopo Ifakara
 Jo Rees, akifundisha mbinu mbalimbali ambazo wakufunzi hawa wanatarajiwa kuzitumia katika kufundishia na hivyo kufanya darasa liwe na uhai na kila mmoja ajisikie huru kuchangia, ni muhimu kuendesha darasa hai, hasa pale unapokua unafundisha mada ambazo zinaonekana kutozungumzwa katika jamii
 Jo Rees, akielezea mfumo wa uzazi wa mwanamke
 Wakufunzi wakisikiliza kwa makini darasa lililokua linaendelea juu ya Hedhi Salama na Ukuaji na mbinu za kufikisha elimu hiyo kwa vijana wa shule za sekondari
 Mkufunzi Elikana akiuliza swali lake kuhusu nini anaweza kufanya endapo kijana shuleni atauliza swali linalohitaji majibu yasiyo wekwa wazi katika kadamnasi ya wanafunzi wengine
 Jo Rees akifundisha mbinu nyingine ambayo inaweza kuongeza uhai wa darasa na kuibua mijadala baina ya wanafunzi wenyewe. Mijadala hii inapaswa kusahihishwa na mkufunzi pale inapoelekea kwenye sintofahamu au kutoka nje kabisa ya agenda.
 Wakufunzi wakiibua mjadala juu ya mitazamo yao ya kile wanachokiamini, wakufunzi hawa walijigawa katika makundi mawili yenye kukubali au kutokubali jambo fulani lililowekwa mbele yao na hapo kila mmoja alitoa mtazamo wake uliomfanya kukubaliana au kutokubaliana na jambo fulani
 Jo Rees alifundisha pia mbinu nyingine ambayo itawasaidia wanafunzi katika kufanya maamuzi sahihi hasa pale wanapoamua kuanzisha mahusiano au katika kuchagua washauri
 Wakufunzi wakifuatilia kwa umakini maelekezo wanayopatiwa
 Mijadala ikiendelea katika makundi mbalimbali
Mmoja wa wakufunzi akielezea wenzake juu ya yale waliyoyachambua katika mjadala mdogo kundini kwake

 Jo Rees, alifundisha pia jinsi ya kuwafundisha vijana kupanga malengo, kuweka nia na kufikiria juu ya changamoto watakazotarajia kuzipitia na jinsi gani wanaweza kupambana na changamoto hizo ili kufikia malengo waliyojiwekea
 Michezo ni moja ya mbinu muhimu mno katika kufanikisha kuendesha darasa hai. Jo alifudisha michezo mbalimbali ambayo iliwafanya wakufunzi wote kushiriki bila kuchoka
Mtazamo na uelewa wa kila mmoja wetu juu ya jambo fulani unastahili kuheshimiwa na kusahihishwa kwa upendo kwa manufaa ya wote. Wakufunzi walipata nafasi ya kuelezea kile wanachokiamini kwa kuweka  maoni yao kwenye visanduku

Wakufunzi wakifanya mchezo mwingine wenye nia ya kujenga ujasiri pale unapoamua kufanya au kutokufanya jambo fulani, mchezo  huu humfanya mchezaji kua na jibu moja tuu lisilojichanganya na kutuma taarifa ya ndio wakati mchezaji alimaanisha hapana

Picha ya pamoja na wakufunzi wabobezi Jo Rees, Ivana Laic na wanafunzi  31 wa masomo ya udaktari katika chuo cha Mt. Francis ambao walipokea mafunzo ya Hedhi Salama chuoni hapo.Bi Hyasintha Ntuyeko, mkurugenzi mtendani wa Kasole Secrets aliungana na wakufunzi hawa wabobezi katika kufanikisha mafunzo haya.
Tuesday, 6 December 2016

Ifakara yajadili juu ya Hedhi Salama

  Dean of studies kutoka chuo cha udaktari cha Mt. Francis akifungua rasmi mdahalo wa hedhi salama chuoni hapo, mdahalo uliowahusisha walimu wa sekondari, wanafunzi ya masomo ya udaktari na madaktari bingwa wa magonjwa ya kina mama
 Mwalimu kutoka shule ya sekondari Benignis akichangia mada
 Dr. Omary kutoka hospital ya Mt. Francis akielezea hali jinsi ilivyo kwa wanawake wanaopata matatizo ya hedhi
 Bi. Regina Kway mwanafunzi St. Francis na trainer wa hedhi salama akifanya presentantion juu ya program ya hedhi salama na ukuaji aliyoiendesha shuleni Benignis
 Mwalimu Kisumo kutoka shule ya sekondari Kilombero akielezea  changamoto za wanafunzi mashuleni juu ya hedhi salama bali pia Mwl. Kisumo alitoa maoni yake juu ya nini kifanyike
Picture ya pamoja na wanafunzi wa St. Francis, walimu wa sekondari na team nzima ya Kasole

Wiki ya usafi wa mazingira nchini yatoa kipaumbele katika Hedhi Salama

 Wiki ya usafi wa mazingira nchini ilitoa kipaumbele katika hedhi salama na kubeba ujumbe wa kitaifa wenye kusisitiza huduma ya vyoo bora kwa kuzingatia mahitaji ya jinsia na umuhimu wake katika Hedhi Salama.
 Dr. Ayoub Mgimba, Chief Medical Officer akifungua rasmi wiki ya usafi wa mazingira nchini
 Bibi Rehema Puluma akitoa maoni yake juu ya kauli mbiu ya wiki ya usafi wa mazingira
 Mheshimiwa Stella Ikupa, mbunge akitoa ufafanuzi juu ya nini kifanyike ili mahitaji ya kijinsia yaweze kua na tija katika ujenzi wa vyoo.
 Bi. Rebeca Budimu kutoka UNICEF pia akitoa maoni yake juu ya wiki ya usafi wa mazingira
 Jo Rees, Menstrual Hygiene expert trainer from Australia akielezea juu ya njia mbalimbali zilizoweza kufanikiwa vizuri nchini Ethiopia ambapo yeye mwenyewe aliweza kufanya kazi na wazawa.
 Bi. Blandina akielezea changamoto mbalimbali zinazowakumba walemavu wa viungo kiasi cha kushindwa kabisa kujisitiri wakati wa hedhi.
Dr. Malebo akitoa matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanywa juu ya Hedhi Salama nchini Tanzania
 Bi. Kimberly Height kutoka shirika la TWESA akielezea changamoto mbalimbali zinazowakumba wakimbizi katika kukabiliana na Hedhi Salama
 Bi. Rehema Puluma akielezea changamoto mbalimbali zinazowakumba wasioona katika kukabiliana na Hedhi Salama
 Mmoja wa washiriki wa mdahalo huu akiuliza swali
Mdau wa Hedhi Salama akiuliza swali pia

Tuesday, 8 November 2016

Mganga mkuu wa wilaya Moshi ahadi kuboresha Hedhi Salama wilayani kwake

 Mganga Mkuu wa wilaya ya Moshi- Dr. Wonanji akiongea katika sherehe za kuhitimisha program ya hedhi salama iliyotekelezwa katika shule nne Moshi-vijijini. Program hii ya hedhi salama ilidumu kwa miezi mitatu wilayani hapo ikitekelezwa na mashirika ya Kasole Secrets na Msichana Initiative kwa ufadhili wa ubalozi wa Marekani
Afisa Elimu Afya wa wilaya ya Moshi, Bi. Conjeta Kessy akizungumza  juu ya mikakati endelevu itakayofanya hamasa iliyoletwa na program ya hedhi salama izidi kudumu katika shule nufaika.

 Bi. Angelina Kahangwa, mmoja kati ya wanafunzi wa udaktari ambao walifundisha wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wilayani Moshi katika program ya hedhi salama, akielezea changamoto na mafanikio waliyoyapata kwa kipindi chote walichokua wakitekeleza mradi
Bi. Hyasintha Ntuyeko, Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets, akiwaaga walimu na wanafunzi katika sherehe za kuhitimisha mradi wa hedhi salama uliokua wa mafanikio makubwa wilayani Moshi