Sunday, 20 December 2015

KASOLE SECRETS YAPATA WAFUNDISHAJI WA KUJITOLEA

Wanafunzi kutoka umoja wa vyuo vya madaktari Tanzania wakipokea vyeti vyao baada ya kumaliza semina ya siku mbili iliyohusu hedhi salama na balehe, wahitimu hawa wanategemewa kwenda kutoa elimu juu ya hedhi salama na balehe katika shule za sekondari za Dar-es-salaam

Jo Rees mtaaluma wa maswala ya afya kutoka Australia akiongea na wakufunzi juu ya hedhi salama na balehe na kuwapa wakufunzi hawa uelewa zaidi na nini wafanye wanapokua wanawafundisha wanafunzi mashuleni juu ya mada hizi nyeti zenye kuathiriwa na tamaduni na usiri mkubwa
Ufundishaji wenye kusisitiza michoro, mijadala katika vikundi vidogo vidogo na uwakilishaji wa mwanafunzi mmoja mmoja katika yale yaliyo jadiliwa kwenye vikundi ni njia moja rahisi sana ya kuwafanya wanafunzi waweze kuvunja ukimya
Michezo inanafasi kubwa katika kuwajengea wanafunzi ujasiri na kuwapa uhuru zaidi wa kusoma pamoja kwa ushirikiano bila kuchekana, kuogopa kuuliza maswali na kuona aibu pale wanapofundishwa kwa pamoja vitu ambavyo tamaduni zao zilizifanya kua siri kubwa na pengine hata kutumia lugha ngumu katika jitihada ya kuviwasilishaNi vyema kuwaelekeza mabinti bila ya kuwaficha ni jinsi gani wanaweza kuzibandika taulo hizi katika chupi zao, wazitupe vipi, wazifue vipi na kuzianika wapi, kwanini ni muhimu kwao kunawa mikono kabla na baada ya kubadilisha hizi taulo, kwanini usafi wao wa mwili, choo na usalama wa maji wanayotumia kunawia na kufulia taulo hizi ni muhimu sana kwaoTunafurahi kufanya kazi pamoja na umoja wa wanafunzi kutoka vyuo vya udaktari Tanzania (TAMSA) wote tukiwa na lengo moja, nia moja na ari ya kuelimisha na kuleta mabadiliko katika jamii nzima hasa katika maswala muhimu ya hedhi salama na balehe yaliyofanywa na tamaduni zetu kua siri na kusababisha utumiaji wa lugha ngumu sana na vitisho katika kufikisha ujumbe kwa walengwa kitu ambacho kimekua kikiendelea kuwaathiri watoto wa kike na wa kiume kwa kiasi kikubwa


0 comments: