Friday, 1 May 2015

MABINTI WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU, WAPATA NAFASI YA KUJIFUNZA JUU YA HEDHI SALAMA

 Binti wa Kijita akielezea mila za wajita kwa binti/mama aliyepohedhi, kua si ruhusa kuonana na baba yako, na unapaswa kukaa ndani huku ukiwa umevaa vazi moja la khanga tuu, mpaka hapo unapomaliza hedhi ndipo ubadilishe vazi hilo
Binti wa kichaga akielezea, jinsi alivyoogeshwa na magadi kwa nguvu, baada ya kuchuma maboga akiwa kwenye hedhi, anasema onyo hilo la kutokuchuma maboga alipewa na bibi yake mara tu alipoingia hedhi, lakini alilazimika kukiuka sharti hilo baada ya kuona amebaki mwenyewe nyumbani na usiku unaingia, hivyo alipaswa kuandaa chakula.
Binti wa Kisukuma akielezea siku ya kwanza alipovunja ungo, alimwambia mama yake, mama yake alimwambia kua asipike wala asiguse vyombo vyake mpaka hapo atakapomaliza, alisisitiza kua mama yake alimwambia shughuli hizo atazifanya tena, mara atakapohakikisha kua amemaliza siku zake.
Binti wa kichaga akielezea jinsi alivyokatazwa kuchuma dawa shambani na mama yake alipokua ameingia hedhi, anasema dada yake alimtuma akachume hiyo dawa shambani, anasema hakujua kama ni mwiko yeye kuichuma hiyo dawa, dada yake alijua kua ni mwiko ndo maana alimtuma yeye, lakini pia dada yake hakujua kama mdogo wake amevunja ungo na siku hiyo kua mdogo wake pia alikua katika siku zake.
 Wa kwanza kushoto ni bibi Consoler Elia, mlezi wa mabinti hawa, katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Kasole Secrets, Hyasintha Ntuyeko, na wa tatu ni mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu


Mabinti wakifurahia zawadi za Glory pads walizopatiwa na kampuni ya Kasole secrets katika maandalizi ya kujiandaa kusherehekea siku ya hedhi duniani, 28 May 2015

0 comments: