Sunday, 20 December 2015

KASOLE SECRETS YAPATA WAFUNDISHAJI WA KUJITOLEA

Wanafunzi kutoka umoja wa vyuo vya madaktari Tanzania wakipokea vyeti vyao baada ya kumaliza semina ya siku mbili iliyohusu hedhi salama na balehe, wahitimu hawa wanategemewa kwenda kutoa elimu juu ya hedhi salama na balehe katika shule za sekondari za Dar-es-salaam

Jo Rees mtaaluma wa maswala ya afya kutoka Australia akiongea na wakufunzi juu ya hedhi salama na balehe na kuwapa wakufunzi hawa uelewa zaidi na nini wafanye wanapokua wanawafundisha wanafunzi mashuleni juu ya mada hizi nyeti zenye kuathiriwa na tamaduni na usiri mkubwa
Ufundishaji wenye kusisitiza michoro, mijadala katika vikundi vidogo vidogo na uwakilishaji wa mwanafunzi mmoja mmoja katika yale yaliyo jadiliwa kwenye vikundi ni njia moja rahisi sana ya kuwafanya wanafunzi waweze kuvunja ukimya
Michezo inanafasi kubwa katika kuwajengea wanafunzi ujasiri na kuwapa uhuru zaidi wa kusoma pamoja kwa ushirikiano bila kuchekana, kuogopa kuuliza maswali na kuona aibu pale wanapofundishwa kwa pamoja vitu ambavyo tamaduni zao zilizifanya kua siri kubwa na pengine hata kutumia lugha ngumu katika jitihada ya kuviwasilishaNi vyema kuwaelekeza mabinti bila ya kuwaficha ni jinsi gani wanaweza kuzibandika taulo hizi katika chupi zao, wazitupe vipi, wazifue vipi na kuzianika wapi, kwanini ni muhimu kwao kunawa mikono kabla na baada ya kubadilisha hizi taulo, kwanini usafi wao wa mwili, choo na usalama wa maji wanayotumia kunawia na kufulia taulo hizi ni muhimu sana kwaoTunafurahi kufanya kazi pamoja na umoja wa wanafunzi kutoka vyuo vya udaktari Tanzania (TAMSA) wote tukiwa na lengo moja, nia moja na ari ya kuelimisha na kuleta mabadiliko katika jamii nzima hasa katika maswala muhimu ya hedhi salama na balehe yaliyofanywa na tamaduni zetu kua siri na kusababisha utumiaji wa lugha ngumu sana na vitisho katika kufikisha ujumbe kwa walengwa kitu ambacho kimekua kikiendelea kuwaathiri watoto wa kike na wa kiume kwa kiasi kikubwa


Friday, 18 December 2015

KASOLE SECRETS YAENDESHA MAFUNZO YA HEDHI SALAMA NA BALEHE

Kampuni ya Kasole secrets inayoendesha mtandao wa hedhi salama, leo wameendesha mafunzo ya hedhisalama na balehe kwa wanafunzi wanaosomea masomo ya udaktari nchini Tanzania, wanafunzi hawa wanategemewa kwenda kutoa elimu hii katika shule za sekondary hapa nchini kupitia programu maalumu ijulikanayo kama Pamoja Tanzania program. Programu hii ya Pamoja Tanzania inalenga kupeleka Taulo za glory katika mashule za sekondari kwa bei ya chini kabisa, huku ikitoa elimu ya hedhi salama na balehe kwa wanafunzi wote wa kike na wa kiume. 
Programu hii ya hedhi salama inafanya kazi pamoja na umoja wa wanafunzi wa vyuo vya udaktari Tanzania, ambao hawa ndio walimu wetu katika mashule, lakini pia muongozo wa ufundishaji unaotumika umeandaliwa na muuguzi Jo Rees kutoka Australia ambaye aliweza kufaulu katika kuutumia muongozo huu vizuri sana katika shule nchini Ethiopia
Hyasintha Ntuyeko, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Kasole Secrets akiwafungua mafunzo ya hedhi salama na balehe

 Dr. Aidat Mugula akitoa mafunzo ya hedhi salama na balehe kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya udaktari Tanzania, ambao wataenda kufundisha elimu hii katika shule za sekondari zilizopo karibu nao
Mdahalo na michango ya agenda kutoka kwa wakufunzi

Wakufunzi wakiwa kwenye makundi  wakijadili na kuchora michoro kuonyesha mabadiliko katika mwili wa binti na kijana na ni kwanini mabadiliko haya hutokea

Michezo ni moja kati ya zana muhimu mno katika kufundishia, wakufunzi wakifanya michezo mabalimbali yenye kufundisha kirahisi na kumfanya mwanafunzi aweze kukumbuka
Dinnah Nyirenda na Lilian Benjamin kutoka Hubert Kairuki Medical School walijishindia taulo za Glory baada ya kuweza kulijaza jedwali lenye kuonyesha mabadiliko ya mwili ayapitiayo bnti na kijana, mchezo huu unajulikana kama puberty bingo